Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA–, Mkuu wa Kundi la Washauri wa Makao Makuu ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Brigedia Jenerali Ali Fadavi, amesema kuwa ushahidi wa Imam Shahidi Sayyid Ali Khamenei umeufanya mwelekeo wa Mapinduzi ya Kiislamu kuwa wazi zaidi, akieleza kuwa ujasiri ulikuwa miongoni mwa sifa zake kuu.
Akizungumza katika mahojiano na televisheni, Brigedia Jenerali Fadavi alisema kuwa Imam Shahidi alidhihirisha ujasiri wa kweli katika maisha yake yote, akibainisha kuwa sifa hiyo ni alama mahsusi ya kizazi cha Imam Husayn (a.s.). Aliongeza kuwa alikuwa akitekeleza majukumu yake ya Kiislamu kwa yakini, imani thabiti na kumtegemea Mwenyezi Mungu kikamilifu.
Fadavi alisema kuwa Imam Shahidi alikuwa na imani kwamba jamii ya Kiislamu inapaswa kufikia kiwango cha juu cha ustaarabu na ukamilifu wa kiroho, huku mazingira yakitayarishwa ili ulimwengu mzima umpokee na kumtambua Imam al-Mahdi (a.f.). Kwa mujibu wake, njia hiyo inaanza kwa kuifahamu na kuifuata shule ya Imam Husayn (a.s.).
Aidha, alieleza kuwa baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Imam Shahidi aliendelea kusimama imara katika njia hiyo bila kuyumba, hadi alipofikia daraja la juu kabisa analoweza kulifikia mwanadamu ambaye si maasumu, nalo ni daraja la ushahidi (Shahada).
Brigedia Jenerali Fadavi alihitimisha kwa kusisitiza kuwa ushahidi wa Imam Shahidi umeimarisha zaidi azma ya kuendeleza malengo ya Mapinduzi ya Kiislamu na umeacha urithi wa ujasiri, imani na msimamo thabiti kwa vizazi vijavyo.
Your Comment